Babu wa miaka 73, aliyemjeruhi vibaya na kusababisha kifo cha mwanawe aliyekuwa mlevi kwa madai ya kutatiza usingizi wake, sasa anazuiliwa na polisi wa lokesheni ya Chepsiro kule Cherangany kaunti ya Transnzoia.
James Tarus alikamatwa baada ya kutekeleza kitendo hicho jana mwendo wa saa moja jioni, kulingana na taarifa ya DCI George Kinoti.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa amerejea nyumbani baada ya miaka minne, ila akawa amepitia vilabuni na kulewa kabla ya kupitiliza hadi chumbani mwa baba yake na kumuamsha kwa lazima.
Akiwa na gadhabu, baba yake aliamka na kumpiga kichwani kwa kipande cha ubao kabla ya kumfunga kwa kamba kwenye kiti.
Wakaazi na chifu wa eneo hilo walipofika eneo la tukio waliupata mwili wa marehemu kwenye kiti alichofungiwa na baba yake, ambaye aliishia kutiwa chini ya ulinzi na polisi wa Cherangany uchunguzi ukiendelea.
Leave a Comment