Mzozo kati ya ndugu na dada nyumbani kwao kule Kwanza kaunti ya Transnzoia, umegeuka kuwa mauti baada ya mwanamme mwenye umri wa miaka 40 kuaga dunia kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye vita hivyo.
Jane Chebor, 48, na ndugu yake Daniel Kipketer, 40, walizozania jambo ambalo halijulikani kabla ya mzozo wao kugeuka vita katika kijiji cha Soyimining “B”.
Kulingana na taarifa ya DCI, Mshukiwa Chebor alidaiwa kutumia fimbo kumgonga nduguye nyuma ya kichwa na muda mfupi akaanza kutokwa na damu mapuani na kuaga dunia.
Mshukiwa Chebor alikamatwa huku polisi wakipata rungu aliyotumia kumuua nduguye, ambaye mwili wake sasa unahifadhiwa kwenye makafani ya hospitali ya rufaa ya Kitale.
Leave a Comment