Mbunge wa Mogotio, Dkt Daniel Tuitoek, amesema mfumo mpya wa elimu maarufu CBC unahitaji kiwango kikubwa cha pesa ,ili kufanikisha utekelezwaji wake na utoaji wa mafunzo shuleni.
Akihutubu katika hafla moja ya elimu katika tarafa ya Kisanana,Tuitoek alisema utekelezaji wa mfumo huo unazidi kukabiliwa na changamoto nyingi,na hasa katika shule zilizoko mashinani.
Tuitoek alisema bunge la kitaifa linapendekeza fedha zaidi kutengwa kwa manufaa ya mfumo huo ikizingatiwa kwamba,shule nyingi hazina vifaa na walimu wa kutosha.
Leave a Comment