Kamishna Raymond Nyeris wa tume ya kitaifa kuhusu haki za kibinadamu alihimiza jamii za wafugaji katika eneo la Baringo kuungana,na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu mikakati za kudumisha amani ya kijamii kaskazini mwa bonde la ufa.
Akihutubu katika lokesheni ya Sandai kwenye eneobunge la Baringo Kusini siku ya Alhamisi,Kamishna huyo alisema wananchi hawawezi kufurahia rasilmali zao pasipokuwa na amani katika jamii.
Kulingana na Nyeris wahalifu wachache wanaharibu sifa bora za jamii Fulani.
Aidha aliwahimiza wazee kutoka kwa jamii zote husika kuwa kwenye mstari wa mbele kujenga amani ya kudumu eneo hilo.
Leave a Comment