Huenda mradi wa ujenzi wa nyumba kwa wale wenye mapato ya chini usitimie baada ya jamii ya Isahakia kudai mahali kunakojengwa mradi huo ni mali yao.
Licha ya serikali ya kaunti ya Nakuru kuanza shughuli ya kuwatafuta wafadhili ili mradi huo uweze kuendelea, jamii hiyo imesema ardhi hiyo ni mali yao waliyopewa na tume ya ardhi nchini.
Mwenyekiti wa jamii hiyo Ali Farah amesema kuwa ni Rais Uhuru Kenyatta pekee ambaye angeteua mzozo wa umiliki wa ardhi baina yao na shirika la utafiti wa kilimo nchini KALRO.
“Sisi tuko na NGO ambayoitajenga hospitali na kilakitu ambacho tunahitaji,hatuhitaji ujenzi wa kaunti kwani ardhi hii ni yetu tuliopewa na Rais.”Ali Farah amesema.
SILAS MWITI
Keep up
Najaribu kusikiliza Kata jasho lakini inasema not streaming