News

Ukosefu wa Hospitali wahatarisha maisha Salgaa

Written by admin

Ukosefu wa hospitali kwenye eneo la Salgaa umetajwa kuchangia pakubwa  kwa vifo vya watu ambao huhusika kwenye ajali na kuhitaji matibabu ya dharura.

Akizungumza kwenye eneo la Boror mbunge wa Rongai Raymond Moi amesema wagonjwa hulazimika kupelekwa kwenye hospitali ya PGH mjini Nakuru huku wengi wakizidiwa barabarani.

Raymond amekiri kuwa aliyekuwa raisi Mwai Kibaki alikuwa ametoa ahadi ya kujenga hospitali kwenye eneo hili la Salgaa huku akiitaka serikali kuitimiza ndoto ya rais huyu mstaafu na kuokoa maisha.

About the author

admin

Leave a Comment