Wakazi wa mtaa wa Kasarani katika eneo la Elburgon wamesema ukosefu wa maji safi katika eneo hilo ni tishio kwa afya ya umma haswa wakati huu ambao kumezuka virusi vya Korona.
Wakiongozwa na mzee Kelvin Mburu wakazi wamesema wao hununua maji kwa shilingi 10 kwa kila mtungi huku kwa sasa watu wakilazimika kunawa kila wakati
Kauli yake imeungwa mkono na Irene Njeri Maina ambaye amesema wenyeji wanaitaka serikali ya kaunti ya Nakuru kuhakikisha wamepata maji safi pamoja na sabuni ya kukabiliana na virusi vya Korona.
Ukosefu huo wa maji pia umetajwa kuwepo mjini Elburgon na viunga vyake huku wanatumia visima wakisema maji hayo hupungua msimu wa kiangazi.
Yakijiri hayo…
Hali ya hofuimetanda katika kijiji cha Karagita mjini Naivasha baada ya mwanamme mmoja kuanguka na kufariki papo hapo.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo wamesema hawana uhakika mwanamme huyo aliugua ugonjwa gani,wakisema walimuona akitembea polepole huku akishilia ukuta na akaanguka na kufariki.Wakazi wameomba serikali kuchunguza kilichosababisha kifo hicho.
Leave a Comment