News

Ukosefu wa madini ya Iron unawafanya dada wawili kula sabuni

Ukosefu wa madini ya Iron ndio unaowafanya dada wawili wa kauti ya Nandi kula sabuni, uchunguzi wa wataalamu wadhihirisha. Picha/lifehealth.com
Written by admin

Imebainika kuwa dada wawili Sharon Chepchirchir  na Lydia Chepkemboi kutoka eneo la Chepterwai kaunti ya Nandi ambao wamekuwa wakila sabuni tangu utotoni mwao wana kiwango kidogo cha madini ya chuma ama Iron mwilini mwao.

Hii ni baada ya wawili hao kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Oak Tree Mjini Eldoret kubaini kinachosababisha wawili hao kula sabuni.

Kwa mujibu wa Mtaalamu wa Masuala ya Figo Dkt. Mathew Koech ambaye aliongoza uchunguzi huo, japo wawili hao huzingatia lishe bora, wamepatikana na kiwango kidogo cha madini hayo jambo ambalo si la kawaida hivyo wataendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Daktari Koech amefahamisha mwandishi wetu kuwa wawili hao hawajaathirika kwa vyovyote na ulaji wa sabuni japo pana uwezekano wakaathirika iwapo wataendelea.

Huyu hapa Sharon Chepchirchir mwenye umri wa miaka 24 akielezea kuhusu mazoea yake na dadake ya kula sabuni tangu utotoni.Wawili hao sasa watasubiri kwa muda uchunguzi zaidi kuhusiana na hali yao ya afya ukiendelea.

Na Judy Jerono

About the author

admin

Leave a Comment