News/Habari

Usalama Baringo: Gavana Kiptis ataka wenyeji kupewa hati milki za mashamba

Kuligana na gavana Kiptis, hati milki za mashamba zitasaidia wakaazi kuwekeza katika biashara zingine na hivyo kusuluhisha tatizo la umaskini na ukosefu wa usalama.
Written by admin

Gavana wa kaunti ya Baringo Stanley Kiptis anasema utoaji wa vyeti vya umiliki wa ardhi utaboresha maisha ya wakaazi wa maeneo bunge ya Tiaty na Baringo Kaskazini.

Kiptis amesisitiza kwamba wakaazi wa maeneo hayo wakipata hati milki hizo, zitawasaidia kufungua milango ya uwekezaji na haswa kwa sekta ya biashara na kilimo.

Akiongea katika lokesheni ya Sabatia kwenye kaunti ndogo ya Koibatek mnamo Jumanne, Kiptis alisema idadi kubwa ya watoto   hawajapata masomo kule Tiaty kutokana na wazazi wao kuwa umasikini.

Kulingana na gavana huyo sekta ya ufugaji pia itaimarika  wakati wakaazi hao watapata hati milki za mashamba, kwani serikali yake itawekeza katika kuwainua kufanya kilimo biashara.

“Baringo north, Tiaty na Baringo South, viongozi tunahitaji ushirikiano mkubwa sana utakaosaidia kubadilisha mawazo ya watu wetu ili kumaliza uhasama wa wizi wa mifugo na kuleta amani. Kwa njia hii tutakuwa tumehakikisha watoto wote waliofikisha umri wa kwenda shule wanasoma pasi na matatizo” Kiptis akasema katika mahojiano  ya kipekee na mwandishi wa idhaa hii.

Na Jeremiah Chamakany

About the author

admin

Leave a Comment