Tume ya
kitaifa ya uwiano na utangamano (NCIC), imewahimiza Wakenya kukubali na
kufurahia tamaduni mbali mbali za humu nchini. NCIC imetoa tamko hilo wakati
wakenya wakiadhimisha siku ya utamaduni ambayo awali iliitwa Moi Day.
Mwenyekiti wa tume hiyo Rev. Samuel Kobia alisema katika ujumbe wake kwamba kujifunza kufurahia utamaduni wa taifa hili ni muhimu kwa jitihada za kudumisha amani hapa nchini.
Alisema kwamba siku hii huwapa wakenya fursa ya kusherehekea tamaduni mbali mbali za humu nchini na pia kujifunza jinsi ya kuvumiliana. Check out our Online Casinos Comparison Guide When it comes to playing poker, there’s nothing like playing at an clickmiamibeach.com Online Poker Room that’s powered by PlayMGM.
Aidha, Kobia aliwataka wakenya kutumia siku hii kwa kujaribu kuwaelewa watu wa makabila mengine hapa nchini kama hatua ya kukuza moyo wa undungu na umoja.
Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i alitangaza Oktoba tarehe 11 kuwa siku kuu kwa vile siku hiyo kuu ya Utamaduni ambayo huadhimishwa tarehe 10 mwezi Oktoba kila mwaka, iliangukia siku ya Jumapili.
Matiang’I alikuwa ametoa wito kwa
wakenya kutambua na kusherehekea utofauti wa tamaduni mbalimbali humu nchini
kwa minajili ya kuhimiza umoja, mshikamano wa kitaifa na ukuaji wa kiuchumi.
Kabla ya katiba mpya kurasmishwa
mnamo mwaka 2010, Oktoba 10 ilikuwa ikiadhimishwa kama Moi Day kwa ajili ya
Rais mtaafu Daniel Arap Moi.
hata hivyo mnamo mwaka 2019, siku
hii ilbadilishwa jina kutoka Moi day na kuitwa Huduma Day lakini baadaye jina
hilo likabadilishwa tena na sasa kuitwa Utamaduni day.
Leave a Comment