News

Vijana 100 wakamatwa kisa barua bandia za kujiunga na Jeshi Eldoret

Written by admin

Vijana zaidi ya 100 walikamatwa hiyo jana baada ya kuripoti katika kambi ya Mafunzo ya kijeshi ya Eldoret wakiwa na barua bandia.

Kulingana na Msemaji wa KDF Koloneli Paul Njuguna, ni kuwa. Kuna uwezekano watuhumiwa walipata barua hizo kutoka kwa walaghai akisema wanatambua tu barua zilizotolewa katika vituo vya kuajiri ambavyo vilikuwa gazetini.

Koloneli Njuguna amesema kuwa, iwapo kulikuwa na uajiri tofauti na iliyofanyika katika kituo hicho, kwa hakika ilikuwa kazi ya walaghai akiongezea kuwa, Kwa bahati mbaya Wakenya wengi waliweza kulaghaiwa.

Msemaji huyo wa KDF amewaeleza wakenya kuwa, shughuli hiyo ya kuwaajiri wanajeshi umekamilika na wasikubali kulaghaiwa na yeyote kuwa shughuli hiyo inaendelea akiongezea kuwa, zoezi hilo lilifanyika katika vituo vilivyokuwa vimetangazwa pekee.

Mwaka jana takriban vijana 70 pia walikamatwa walipojitokeza katika Shule ya Mafunzo ya makurutu mjini humo-RTS na barua ghushi.

Walishtakiwa kwa makosa mawili ya kughushi, wakiwa na barua ya kughushiwa na kuwasilisha hati bandia katika shule hiyo.

Judy Cherono

About the author

admin

Leave a Comment