News

Vilabu kufungwa Salgaa kwa kuhatarisha usalama

Afisa wa polisi wa utawala AP amwaga pombe haramu eneo la Molo tarehe 6 Oct,2019. Vilabu kadhaa vimefungwa eneo la Salgaa kwa kuhatarisha usalama. Picha/ Bernard Waweru/SYM

Serikali ya kaunti ya Nakuru inaendeleza oparesheni dhidi ya vilabu ambavyo vinachangia katika kuzorota kwa usalama wa maeneo mbali mbali katika eneo bunge la Rongai.

Hii ni kwa mujibu wa msimamizi wa gavana kaunti ndogo ya Rongai Ben Yatich ambaye amesema kwamba, baadhi ya vilabu katika maeneo ya lusaka, Salgaa na Rongai vimekuwa vikitumika na wahalifu kama mafichio.

Akizungumza katika mkutano wa baraza eneo la Kampi ya Moto Alhamisi, Yatich alidokeza kuwa tayari kamati ya kudhibiti vileo kaunti ndogo ya Rongai imefunga vilabu kadhaa katika eneo la Lusaka na Salgaa, kwa  kuwa tishio kwa usalama wa wenyeji.

Tunashirikiana na maafisa wengine 11 ikiwemo wale wa afya na naibu kamishna wa hapa Rongai kwa ajili ya kuhakikisha vilabu vinavyohudumu ni vile ambavyo vimeafiki vigezo tulivyowekaā€¯ Yatich akasema

Haya yanajiri wakati ambapo naibu Chifu wa eneo la Soin katika eneo la Sachagwan Robert Keter anashukiwa kuwadunga kisu na kuwajeruhi watu wanane kwa muda wa mwezi mmoja unusu.

Naibu kamishina wa kaunti ndogo ya Molo David Wanyonyi alisema baada ya kuwasiliana na kamishina wa kaunti ya Nakuru Erustus Mbui hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya chifu huyo.

Miriam Itotia na Bernard Waweru

About the author

admin

1 Comment

Leave a Comment