Wawakilishi bunge kutoka kaunti ya Baringo wamemkashifu mbunge wa Tiaty William Kamket kwa matamshi aliyoyatoa siku ya Jumamosi akitaka idara ya uchunguzi wa jinai kumchunguza naibu rais William Ruto kuhusu kashfa ya silaha inayomkumba aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa.
Wakizungumza mjini Eldoret, mawakilishi bunge hao wamemkemea mbunge huyo huku wakisema kuwa, kamket amekuwa na mazoea ya kumuongelea naibu rais kwa njia ya kumharibia jina wakisema sharti akome la sivyo atasababisha utengano miongoni mwa wakenya.
Wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la baringo Lawi Kipchumba Tallam, na mwakilishi wadi ya Bartabwa Reuben Chepsongol, wamemtaka Kamket kumheshimu naibu rais na kutoingiza kila jambo katika siasa.
Haya yanajiri wakati pia viongozi wa upinzani wakimtaka naibu rais kueleza ni vipi afisi yake ilitumika katika biashara hiyo ya zabuni ghushi ya shilingi bilioni 40 ya silaha.
Leave a Comment