News

Visa vya kujitoa Uhai Nyandarua vyatisha

Written by admin

Visa vya watu kujitoa uhai katika kaunti ya Nyandarua vimeendelea kushuhudiwa, kisa cha hivi karibuni kikiwa cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 31 kutoka Kijiji cha Gatitu Kinangop Kusini.

Mwili wa mwanamume huyo kwa jina Samuel Nderitu Wanjohi ulipatikana ukiwa umening’inia katika shule ya Chekechea ya Kakongo Mita 200 kutoka nyumbani kwao.

Kulingana na ripoti ya polisi mkewe mwendazake pamoja na marafiki ndio waliompata mwanamume huyo akiwa amejitoa uhai  jana  baada ya kukosa kurejea nyumbani.

Aidha mkewe mwendazake amesema kuwa Mumewe alionekana mwenye msongo wa mawazo kwa kupoteza kazi yake kufuatia janga la Covid-19. Maafisa wa polisi walifika katika eneo la tukio na kuupeleka mwili wa mwendazake katika ufuo wa hospitali ya Engineer kwa upasuaji.

Kwingineko ……….

Wakazi wa eneo la Huhoini Kwa Ngegi Kata ndogo ya Nyandarua Magharibi wanataka uchunguzi wa kina ufanywe baada ya mwanamme mmoja aliyekamatwa akiwa mlevi kujitoa uhai katika seli ya kituo cha polisi cha Huhoini.

Inadaiwa kuwa Simon Ngaruiya Muhia alijitoa uhai kwa kujinyonga akitumia shati lake ila wakazi hao wametilia shaka jambo hilo kuona kituo hicho kulikuwa na maafisa wa polisi.

David Kinyajui ambaye ni nduguye mwendazake amesema kuwa Simon amekuwa akilewa na kurushia cheche za maneno wakazi ila hakuwahi kumdhuru yeyote huku ulevi wake ukimfanya atiwe mbaroni Mara kwa Mara.

Akidhibitisha kisa hicho Mkuu wa polisi katika kaunti ya Nyandarua Zachary Kimani amesema kuwa mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika ufuo wa hospitali ya rufaa ya Nyahururu ukitarajiwa kufanyiwa uchunguzi na madaktari.

About the author

admin

Leave a Comment