News

Wafanyibiashara wa Uganda matatani, bidhaa gushi zaendelea kukamatwa

Washukiwa sita wa ulanguzi wa watoto wakamatwa.
Written by admin

Wafanyabiashara zaidi ya hamsini kutoka nchi jirani za Tanzania na Uganda walizuiliwa kwa zaidi ya  saa sita hiyo mnamo Ijumaa na maafisa wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA mjini Eldoret, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuingiza bidhaa humu nchini bila ya kulipia ushuru.

Baadhi ya bidhaa zilizonaswa ni pamoja na viatu, unga na mavazi, vyote ambavyo vilikuwa kwenye basi lenye nambari za usajili za Uganda na zilikuwa zikisafirishwa kuelekea jijini Nairobi kutoka Kampala.

Baadhi ya wasafiri na wafanyibiashara hao walielezea masikitiko yao na jinsi shughuli hiyo inavyoendelezwa na kuelezea kuwa wamelipia ushuru na kushindwa sababu kuu ya kuzuiliwa kwao kwa zaidi ya saa sita.

Juhudi za mwandishi wetu kuzungumza na meneja wa KRA tawi la Eldoret ziligonga mwamba.

About the author

admin

Leave a Comment