News/Habari

WAFANYIKAZI WA SHULE YA NAKURU HILLS WADAI KUDHULUMIWA, KUNYIMWA MSHAHARA MIEZI 8.

Wafanyikazi wa shule ya spesheli ya Nakuru Hills iliyoko eneo la London viungani mwa mji wa Nakuru  jana waliandamano wakilalamikia  kukandamizwa na kucheleweshwa kwa mishahara yao.

Wafanyikazi hao   hawajapokea malipo yao ya tangia mwezi Agosti mwaka jana.

Wakiongozwa na Tom Nandi wamelaumu usimamizi wa shule hiyo kwa kutojali maslahi ya wafanyikazi na kutaka wizara ya elimu kuingilia kati.

Usimamizi wa shule hiyo unasema kuchelewa kwa mishahra hiyo kunatokana na utaratibu mrefu kwenye serikali    japo wamekana madai ya kukandamiza wafanyikazi.

Na Sarah Nyangeri Chege

About the author

admin