News

Wakaazi wa Njoro wahofia kaburi litafukuliwa na mafuriko

Written by admin

Wakaazi wanaoishi maeneo yanayopakana na kaburi  la Njoro la Kang’ari wanaishi kwa hofu  kufuatia mvua nyingi na mafuriko wanayosema yanaweza  kufukua na kufanya miili kwenye kaburi hilo kuelea.

……huku hayo yakijiri

Mwalimu   mmoja mwenye umri wa miaka 37  wa  shule ya upili huku Njoro  amekatakatwa hadi kufa na jamaa   mmoja kufuatia kile kinaaminika kuwa mzozo wa shamba eneo la  Tuyoibei  Emitik huko Kuresoi Kusini.

Kulingana na chifu wa Emitik David Cheruiyot,  mwalimu huyo  alifika kwenye shamba lake na kutofautiana na jamaa wanayepakana katika shamba hilo   tukio lililopelekea jamaa huyo  kumkatakata   mwalimu huyo kwa upanga aliokuwa nao.

Juhudi za wananchi hata hivyo za kumkimbiza hospitalini Mwalimu huyo  hazikufua dafu kwani  aliaga dunia alipofikishwa kwenye kituo cha matibabu cha Olenguruone.

Chifu Cheruiyot anasema mshukiwa ambaye amekamatwa na polisi amekuwa na mizozo  na watu wengi katika  eneo hilo.

About the author

admin

Leave a Comment