Wakazi wenye hasira katika kijiji cha Rachong eneo bunge la Ndhiwa wameteketeza nyumba sita za mshukiwa mmoja wa ushirikina.
Kulingana na wakazi hao,mshukiwa Gabriel Osaso, 79 amemfuga mamba anayesemekana kuwahangaisha watu wanaovuka mto kuja.
Haya yanajiri baada ya mamba huyo kusemekana kumwangamiza msichana wa darasa la kwanza alipokuwa njiani kuelekea shuleni siku ya Ijumaa.
Juhudi za chifu wa eneo hilo Joseph Ogur kujaribu kuingilia kati ziliambulia patupu kwani yeye pia alishambuliwa na wakazi waliokuwa na hasira.
Mkuu wa polisi kwenye eneo hilo Dishon Chadaka amewaonya wannachi dhidi ya kuchukua hatua mikononi mwao.
Chadaka anasema mshukiwa kwa sasa anazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Ndhiwa akiendelea kuhojiwa.
Leave a Comment