Shangwe na nderemo zimetawala katika shule ya upili ya nyakiambi katika eneo la Elburgon baada ya mwanafunzi ambaye alipata alama 277 katika kcpe kupata A- katika kcse
Baada ya matokeo hayo kutolewa rasmi na waziri wa elimu Prof George Magoha wakazi wa eneo la Arimi na Nyakiambi waliweza kujitokeza na kusherehekea mwanafunzi huyo bora katika eneo hilo
Samson Gachie Muchai mwenye umri wa miaka 17 amesema nidhamu pamoja na bidii imemwezesha kuzoa alama ya A-
Mamake akiongoza wenyeji wa eneo hilo amesema juhudi zao zimeweza kuzaa matunda huku akisema mwanawe hudumisha viwango vya juu vya nidhamu.
Leave a Comment