Wakulima wametakiwa kuepuka kutumia moto kutayarisha mashamba yao kwa upanzi, mbinu hii ikitajwa kuwa hatari kwa mazingira na hata wananchi kwa jumla.
Akizungumza katika eneo la Salgaa mwakilishi wa wadi ya Mosop Daniel Mutai amesema kwamba, upepo ulioko unaweza kufanya moto kusambaa na kuleta maafa.
Amedokeza kuwa, baada ya uchunguzi amebaini kuwa wakulima wengi wanatumia mbinu hii kwenye mashamba yao jambo ambalo halifai.
Kulingana na mutai, mbinu hii ya moto ilisababisha hasara chungu nzima kwenye miaka ya hapo awali baada ya kuchoma nyumba za watu na hata nyasi mashambani.
Leave a Comment