Huku msimu wa Krismasi ukiwadia, wakenya wa tabaka mbalimbali wataungana na ulimwengu kuadhimisha siku hii,viongozi wa kundi moja la walemavu kwenye kaunti ndogo ya Koibatek wanasema ukosefu wa pesa utawafungia nje walemavu wengi ambao wangependa kuadhimisha siku hiyo ,kama wakenya wengine.
Wakiongozwa na John Ng’etich ambaye amezungumza kwa niaba ya watu wanaoishi na changamoto za kimaumbile kwenye kaunti ndogo ya Koibatek,viongozi hao wanasema kwa kipindi cha miezi 6 ambazo zimepita,walemavu katika eneo hilo hawajapokea marupurupu yao ya shilingi elfu 2 kutoka kwa serikali ya Baringo..
Afisa msimamizi wa serikali ya kaunti kwenye wadi ya Eldama Ravine Bismark Koske anasema ingawa malipo hiyo imeonekana kuchelewa kwa wakati huu,walalamishi hao ni sharti watapokea marupurupu zao ikiwemo bima afya kuambatana na mwongozo uliowekwa…
Wakati wa sherehe za Mashujaa mwaka wa 2019 mjini Eldama Ravine,askari wa mji walimpiga bwana John Ng’etich Serian,na kumzuia kutoa lalama zake kwa Gavana Stanley Kiptis kuhusu pesa za walemavu kukosa kusambazwa kwa wote ambao waliweza kusajiliwa.
Leave a Comment