News/Habari

Wanabiashara wa mbao wamkashifu Waziri Tobiko

Written by admin

 Baadhi ya wanabishara wa kupasua mbao katika eneo bunge la Eldama Ravine sasa wamemshutumu vikali waziri wa mazingira nchini Keriako Tobiko,kwa madai ya kuwaadhibu kibiashara kupitia kwa hatua yake ya kuongeza mda wa marufuku ya kuvuna miti, kwenye misitu za serikali.

William Biwott ambaye anaendesha biashara hiyo katika kaunti ndogo ya Koibatek anasema, wanabiashara wa kupasua mbao wanakabiliwa na wakati mgumu zaidi kiuchumi,kwani hawana uwezo wa kulipa mamalioni ya pesa wanazodiwa na mashirika mbalimbali za kifedha,pamoja na benki.

Julius Chesaro ambaye pia anahusika katika biashara ya kupasua mbao anasema waziri Tobiko anafaa kusikia malilio ya wadau hao wa misitu ambao pia wanachangia pakubwa katika sekta ya uajiri humu nchini..

Lalama za aina hii pia zimeshika kasi katika maeneo ya Meru,Laikipia na Nyeri ambapo wanabiashara wa kupasua mbao wametisha kuishtaki shirika la misitu nchini KFS,kwa madai kwamba shirika hilo lina deni lao la shilingi 93 walizokuwa wamelipa kama ada ya kununua miti za kukata kwenye misitu za serikali.

KFS kufikia sasa imetoa taarifa ya kukanusha kuwa na deni lolote la wanabiashara hao wa kupasua mbao,na badala yake kutaka wanabiashara hao kupeleka lalama zao kwa afisi za shirika hilo zilizoko

About the author

admin

Leave a Comment