News

Wananchi waomba uwazi kwa ugavi wa hela

Written by admin

Serikali ya kaunti ya Nakuru imetakiwa kutumia fedha ambazo zimetengwa kupambana na virusi vya corona kwa uwazi na uwajibikaji mkubwa.

Kwa mujibu aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Kamara kwenye bunge la kaunti ya Nakuru Joseph Ngware Ng’ang’a mamia ya wananchi katika kaunti hiyo hawawezi kukidhi mahitaji yao ya kila siku baada ya kushuka kwa mauzo katika biashara.

Kiongozi huyo aidha amemtaka rais Uhuru Kenyatta kujitokeza na kutoa mwelekeo kuhusu hali ya kiuchumi nchini akisema wananchi wanahitaji msaada ili kuendelea na maisha yao kama kawaida……huku  hayo yakijiri …

Wananchi wameombwa kutii na kuzingatia kanuni ambazo zimetolewa na wizara ya afya katika kuzingatia usafi, ili kujiepusha na maambukizi ya kirusi cha Covid-19.

Akiongea na kituo hiki mwakilishi wadi ya Kiamaina Isaack Wahome, amesema kuwa ni muhimu sana kufuata maagizo hayo ya wataalamu wa afya,kama njia moja ya kuzuia kuenea zaidi kwa maradhi hayo.

Wakati huo huo, amewarai wakaazi kutilia maanani amri ya kutotoka nje baada ya saa moja jioni, ili kujiepusha na mashtaka ya kukaidi sheria hiyo.

.                     

About the author

admin

Leave a Comment