Wakazi ambao wanaishi karibu na msitu wa Mau wameelezea hofu yao huku waziri wa mazingira Keriako Tobiko akitarajiwa kuzuru eneo hilo jumapili
Hofu imewaingia wakazi wa eneo la Kapsinedet, Kiptunga na Marioshoni huku waziri wa mazingira Keriako Tobiko akitarajiwa kuzuru eneo hilo siku ya jumapili
Wananchi hao wakiongea katika kituo cha kibiashara cha Kapsinendet wamesema hofu yao ni kufurushwa kutoka eneo hilo katika harakati za serikali kuokoa msitu wa Mau
Wakazi hao wamesema walipata ardhi kutoka kwa serikali wakisema tangu waziri huyo kutangaza mapango wa kufurusha wananchi wamekuwa hofu kubwa tangu mwaka jana
Aidha wamesema wanaunga juhudi za serikali kupitia wizara ya mazingira kupanda miti katika msitu wa Mau na maeneo ya chemchemi
Hata hivyo naibu kamishina David Wanyonyi amewataka wanchi kuondoa hofu iliyopo
Leave a Comment