Muungana wa akina mama wanaoishi na virusi vya ukimwi kwenye eneo bunge la Rongai, umetoa wito kwa serikali kutowabagua watu walio na virusi hivyo haswa wakati wa utoaji wa ajira.
Wakitaka majina yao kubanwa, akina mama hao wamesema kwamba, wamekubali hali yao ya afya na kujiunga kwenye muungano huu ambao unawasaidia kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi.
Kulingana nao, licha ya baadhi yao kuwa wajane wameweza kujifunza mafunzo ambayo yanawawezesha kupata riziki.
Wametoa wito kwa serikali kuwakumba na kuwasidia na ufadhili ambao utawasaidia kuanzisha miradi ambayo itaboresha maisha yao.
Leave a Comment