Wachuuzi na wenye biashara ndogo ndogo mjini Nakuru wameitaka serikali ya kaunti ya Nakuru chini ya Gavana Lee Kinyanjui kurejesha uchukuzi wa matatu katikati pa mji wa Nakuru.
Hii ni baada ya serikali kuu kutangaza kufunguliwa kwa uchumi na kutupiliwa mbali kwa saa za kafyu.
Wachuuzi na wanabiashara hao walisema biashara zao zilikuwa zikitegemea abiria na wamekuwa wakikadiria hasara kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Waliongeza kuwa, kuanguka kwa sekta ya matatu katika kaunti ya Nakuru kumechangia kufirisika kwa baadhi ya kampuni za uchukuzi ambazo zilikuwa zinategemea mikopo.
Zaidi ya yote wametishia kushiriki maandamano iwapo ombi lao litapuuzwa.
Leave a Comment