Washukiwa sita wa kike wanaoaminika kuendeleza biashara
ya ulanguzi wa watoto wamekamatwa na maafisa wa upelelezi Katika kaunti
ya Uasin Gishu wakiwa na watoto wawili wavulana wa Kati ya umri wa miaka
2 na 3.
Akithibitisha
haya,mkuu wa upelelezi Kaunti hiyo Isaac Onyango anasema waliweza
kuwanasa Washukiwa hao kupitia kwa ushirikiano wao na maafisa wa polisi
katika Kaunti ya Kisii.
Bw.Onyango
ameongeza kuwa sita hao wamekuwa wakiendeleza biashara hiyo kutoka
Kaunti moja hadi nyingine huku akitoa mwito kwa jamii kuwa macho kwa
wanao na kuwapa ushauri familia ambazo hazijajaliwa kupata watoto
kutonunua watoto kwa watu wasiowafahamu bali wafike katika makaazi ya
kuwalea mayatima na kufuata masharti yanayoitajika.
Sita hao watafikishwa mahakamani pindi tu maafisa hao watakapokamilisha uchunguzi wao.
Leave a Comment