News/Habari

Wateta Stegi ya Magari

Written by admin

Muungano wa wamiliki wa magari ya matatu kutoka  eneo la Magare Rongai, umeitaka serikali ya kaunti ya Nakuru kurejesha kituo cha kuabiri magari cha maeneo ya Kampi ya Moto, Magare, Mogotio na Eldama-Ravine, kati kati ya mji wa Nakuru.

Mwenyekiti wa muungano huu Fredrick Tanui Timbaktu, amesema kwamba wakongwe wengi kutoka maeneo haya, wamekuwa wakipotea mjini Nakuru na mizigo yao kuibwa kutokana na umbali wa kituo hiki, kilichoko katika sehemu ya chini ya mji huu.

Kulingana naye, tayari muungano huu umeandika ripoti ambayo inapaniwa kufikishwa kwa gavana wa kaunti ya Nakuru Lee Kinyanjui,ili kuleta afweni kwa wakongwe wengi na hata wanafunzi.

Miriam Itotia

About the author

admin

Leave a Comment