News/Habari

Watu wawili wakamatwa kwa usafirishaji haramu Nakuru

Watu wawili wakamatwa Rongai Nakuru kwa usafirishaji haramu
Written by admin

Watu Wawili wanazuiliwa na maafisa polisi katika kituo cha polisi cha menengai rongai kaunti ya Nakuru kwa usafirishaji wa bidhaa aina ya ethanol ya Lita 1630, ambayo hutumika kutengeza pombe haramu.

Ocpd wa rongai kaunti ya Nakuru Wilberforce Sicharani alisema dereva kwa jina la Douglas Waweru alikuwa anafuatwa kutoka kituo cha kibiashara cha salgaa Hadi kwa boma la mwenye gari hilo aina ya pick up Isuzu dmax, kijijini rongai John ndungu Macharia, na kisha akatoroka.

Aidha bidhaa hiyo iliyokuwa imepakiwa kwenye mitungi 60 ya jerican, itakaguliwa na mafisaa wa KRA, kabla ya Wawili hao kufikishwa mahakamani hapo kesho ,siku ya jumatatu tarehe 22 agosti mwaka huu.

About the author

admin

Leave a Comment