Mwakilishi wa gavana kwenye eneo bunge la Bahati Samuel Macharia Wamae, amewaonya wafanyibiashara wa pombe wanaohudumu kinyume cha sheria kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.
Akiongea katika eneo la Maili Kumi, Wamae amesema kuwa imebainika kuwa wengi wa wafanyibiashara hawana leseni za biashara hiyo, jambo ambalo halijakubaliwa kisheria.
Aidha, amesema kuwa ofisi yake kwa ushirikiano na ofisi ya naibu kamishna wa Bahati, imeweka mikakati ya kufanya msako mkali na hata kufunga biashara zisizo na leseni, hasa wakati huu wa shamra shamra za sikukuu ya krismasi.
Leave a Comment