Baadhi ya wazazi wamewasilisha ombi katika Bunge la Kitaifa wakitaka kusitishwa kwa utekelezaji wa Mtaala wa CBC.
Hayo yanajiri licha ya rais Uhuru Kenyatta na waziri wake wa elimu Profesa George Magoha kuendelea kusisitiza kwamba mtaala huo wa umilisi ni bora na wenye manufaa kwa watahiniwa,
Wazazi hao wamewasilisha ombi hilo kupitia kwa Mbunge Maalum Wilson Sossion ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa muugano wa kutetea maslahi ya waalimu (Knut), wakidai utekelezaji wa CBC unakiuka sheria.
Wazazi hao wanapendekeza kushtakiwa kwa maafisa wa serikali ambao wamekuwa wakiendeleza utekelezaji wa mtaala huo mpya kwa kuvuruga ubora wa elimu nchini.
Leave a Comment