News

Wazazi walaumiwa kwa kutowajibika

Written by admin

Huku serikali ya kaunti pamoja na washikadau wa elimu wakiendelea kubuni njia za kuboresha viwango vya elimu nchini, kutowajibika kwa baadhi ya wazazi kumetajwa kama mojawapo ya mambo yanayotishia elimu ya wasichana.

Akiongea katika eneo la Tetu ndani ya kaunti ndogo ya Subukia Janet Otieno mtetezi wa haki za watoto, amedai kuwa wazazi hasa kina mama wamezembea katika majukumu yao, hali ambayo imepelekea wasichana wengi kuolewa wakiwa na umri mdogo na hata kuacha masomo yao kutokana na mimba za mapema.

Aidha, amewataka wazazi kuchukua jukumu la kuwashauri na pia kuwaelimisha wasichana wao, ili kuwaepusha na majanga hayo.

WARUKIRA MWANGI

About the author

admin

Leave a Comment