Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya
kilimo kwenye bunge la kitaifa na pia Mwenyekiti wa Nacada John Mututho,
ameitaka idara ya uchunguzi(DCI) kuwakamata wamiliki wa viwanda ambavyo
vimekuwa vikisiaga unga wenye sumu ya Aflotoxin, kwani hiyo ni njia ambayo
inaweza kuleta maafa nchini.
Kwenye kikao na wanahabari mjini
Nakuru, Mututho amesema kuwa wamiliki hao wanapaswa kuwa wamekamatwa huku
uchunguzi ukiendelea, kwani KEBS tayari imehakikisha kuwa unga huo una sumu.
“Si kazi ya Uhuru kuwakamata waliohusika bali Rais ana mamalaka ya kuamuru wanaouza mahindi na unga wenye aflatoxini watiwe mbaroni mara moja na kufikishwa mahakamani,waziri Kiunjuri na Sicily Kariuki wanafaa kuwa tayari wako nje ya serikali . You can assign roles to your users https://clickmiamibeach.com/ and then map those to a domain class. ”Mututho amesema
Ameongeza kuwa ni wakati ambao Rais
Uhuru Kenyatta anafaa kumfuta kazi waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri pamoja na
waziri wa afya Sicily Kariuki, kwani walipaswa kuwa mstari wa mbele kutangaza
janga Hilo…
Aidha, amesema kuwa mawaziri hao
wamekosa kuwajibika kazini, kwani si Mara ya Kwanza wizara hizo zmekuwa
zikihusishwa kwenye makosa, huku akiwataka wananchi kutokula unga huo kamwe.
Sarah
Nyangeri
Leave a Comment