Wabunge wa bunge la kitaifa la 13, wamemchagua Moses Masika Wetangula kuwa spika mpya wa bunge hilo.
Hata baada ya kukosa kuafikia hitaji la thuluthi mbili ya kura zilizopigwa, Wetangula alitangazwa mshindi baada ya mshindani wake wa karibu Kenneth Marende kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.
Seneta huyo wa zamani wa Bungoma, alipata kura 215 kati ya kura 346 zilizopigwa dhidi ya mshindani wake Kenneth Marende aliyepata kura 130.
Marende ambaye ni spika wa zamani wa bunge la kitaifa, alidinda kushiriki katika awamu ya pili ya upigaji kura, na kumuacha Wetangula kuwa muwaniaji wa pekee.
Seneta huyo wa zamani wa Bungoma, anachukua wadhifa huo kutoka kwa Justin Muturi, aliyeshikilia wadhifa huo tangu mwaka 2013.
Leave a Comment