Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero amewasilisha ombi la kupinga ushindi wa Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga.
Kidero na mgombea mwenza wake Elijah Kodo wamewasilisha ombi hilo mbele ya Mahakama Kuu ya Homa Bay, wakitaka matokeo ya uchaguzi yafutiliwe mbali kwa madai ya ubovu wa uchaguzi.
Katika maombi yake, Kidero anaitaka mahakama kuagiza kuchunguzwa kwa kina kwa nyenzo zote za uchaguzi zikiwemo stakabadhi za kielektroniki, vifaa vya uchaguzi wa ugavana.
Katika kesi hiyo, walalamishi hao wameshtaki Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Msimamizi wa Uchaguzi wa Kaunti hiyo Fredrick Apopa, gavana gladys Wanga, Naibu Gavana Oyugi Magwanga na chama cha O.D.M.
Walalamishi wanahoji kuwa uchaguzi wa ugavana ulikumbwa na dosari, wakiongeza kuwa haukuwa huru wala wa haki kinyume na matakwa ya kikatiba. Vile vile, huko Narok, alyekuwa mgombeaji wa ugavana wa Azimio, Moitalel Ole Kenta, ambaye alishindwa katika uchaguzi uliokamilika, amewasilisha ombi la kupinga kuchaguliwa kwa Gavana Patrick Ole Ntutu.
Akiwa pamoja na timu yake ya wanasheria, amewasilisha ushahidi kupinga ushindi huo na baadae kutangazwa kwa Ntutu wa (democratic alliance) kama gavana.
Leave a Comment