Gavana wa kuanti ya Nakuru, Lee Kinyanjui, amesifia hatua ya baadhi ya makanisa kupiga marufuku wanasiasa kuzungumza kanisani.
Akizungumza na kituo hiki Lee amesema kuwa kanisa ni pahali patakatifu panapofaa heshima kutoka kwa viongozi na kila mtu.
Kiongozi huyo pia amesema baadhi ya wanasiasa wametumia raslimali zao kuhujumu kanisa kupitia michango mikubwa inayokusudiwa kuhadaa waumini na kuharibu maadili ya nyumba za ibada.
Kinyanjuia anawarai viongozi wanaotaka kuuza sera zao kufanya hivyo baada ya vikao vya kanisa ama katika vikao mbadala.
Leave a Comment