Gavana wa Kaunti ya Baringo Benjamin Cheboi amezuru hospitali ya kaunti ndogo ya Eldamaravine siku chache tu baada ya kuapishwa.
Cheboi anasema kuwa hali ya afya imezorota katika kaunti nzima ya Baringo huku akidai kwamba uhaba mkubwa wa dawa unakumba vituo vingi vya afya.
Pia anasema hospitali ya kaunti ndogo ya Eldama Ravine haina nafasi ya kutosha kwa wagonjwa wa kulazwa, kwani wagonjwa wawili wanalazimika kutumia kitanda kimoja.
Cheboi anasema atashirikiana na waakilishi wadi wote wa kaunti hiyo, ili kuimarisha sekta ya Afya katika kaunti ya hiyo Baringo.
Leave a Comment