Kamishna wa kaunti ya Nakuru Erustus Mbui, amewataka wakaazi kutoka kaunti ya Nakuru kuepukana na wanasiasa wanaoendeleza siasa za chuki kwa malengo ya kujitafutia umaarufu.
Akizungumza kwenye eneo la Solai ndani ya eneo bunge la Rongai, Mbui alisema wananchi hawapaswi kugawanyishwa na wanasiasa haswa wakati huu ambapo taifa linaelekea kwa uchaguzi.
Aliongezea kuwa tayari wanasiasa wameanza kuonekana mashinani wakijipigia debe kabla ya uchaguzi mwaka ujao.
Leave a Comment