Wabunge wa Njoro Charity Kathambi wa Gilgil Martha Wangari , wa Naivasha Jane Kihara na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Nakuru Liza Chelule wameomba uwepo wa usalama wa kutosha kwa kina mama watakaowania viti vya kisiasa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongea kwenye hafla moja Nakuru walisema kuwa kina mama hupokea dhulma za aina mbalimbali hususan nyakati za kampeini wakiomba serikali kupitia idara ya usalama hususan katika bonde la ufa kuwahakikishia usalama wao.
Aidha wakiwataka wawaniaji wenza wa jinsia ya kiume kutotumia siasa kushusha hadhi za kina mama hao bali kuuza sera kwa wapiga kura ili kuwezesha ushindani wa haki na kweli.
Walisema haya huku kampieni zikishuhudiwa kuanza nchini, chini mwaka mmoja uchaguzi kuandaliwa.
Leave a Comment