Viongozi wa akina mama katika eneo bunge la Baringo Kaskazini wanataka serikali kuwatambua wanawake ambao ni wajane kama kundi maalum katika jamii, ili kuwawezesha kupokea huduma za kimsingi kutoka kwa serikali na pia mashirika ya wahisani.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa taarafa ya Bartabwa kwenye eneo bunge hilo la Baringo Kaskazini, Rael Chelimo alisema idadi ya wajane katika jamii inazidi kuongezeka, na haswa katika maeneo ambayo yamekumbwa na utovu wa usalama.
Alisema kando na changamoto za uhaba wa vyakula wakati wa ukame, akina mama ambao ni wajane pia wanahitaji kutambuliwa kama kundi spesheli katika utoaji wa basari za kusomesha watoto wao.
Leave a Comment