Sports/Michezo

Australia yamteua Guus Hinddink kusaidia katika maandalizi ya Kombe la Dunia.

Hiddink
Written by admin

Australia imemteua aliyekuwa kocha wa timu ya taifa hilo Guus Hiddink, kusaidia katika maandalizi ya Kombe la Dunia.

Aidha mkufunzi huyo wa Uholanzi alialikwa kuhudhuria mechi yao ya mwisho nyumbani kujitayarisha kushiriki kwa fainali hizo.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye aliiwezesha Australia kupata nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 32, mwaka 2006 ambapo walifuzu kwa mechi za 16 bora, atafanya kazi pamoja na kocha Graham Arnold kwenye mechi dhidi ya New Zealand itakayochezwa mjini Brisbane tarehe 22 Septemba.

Fainali za mwaka huu za kombe la dunia zitaandaliwa nchini Qatar baina ya tarehe 20 Novemba na tarehe 18 Desemba.

About the author

admin

Leave a Comment