Klabu ya Manchester United itachuana na Real Sociedad huku Arsenal ikimenyana na mabingwa wa zamani PSV Eindhoven katika hatua ya makundi ya kombe la Europa.
Vijana wa Erik ten Hag pia watachuana na FC Sheriff na Omonia Nicosia katika kundi E, likionekana kuwa kundi rahisi kwa miamba hao wa Uingereza.
Arsenal pia wamepangwa pamoja na Bodo/Glimt na FC Zurich katika kundi A.
Washindi wa makala ya kwanza ya Europa Conference League Roma kutoka Italia, wamepangwa kundi C pamoja na Real Betis, Ludogorets and HJK.
Droo kamili ya hatua ya makundi
Kundi A: Arsenal, PSV Eindhoven, Bodo/Glimt, FC Zurich
Kundi B: Dynamo Kyiv, Rennes, Fenerbahce, AEK Larnaca Kundi C: Roma, Ludogorets, Real Betis, HJK Helsinki
Kundi D: Braga, Malmo, Union Berlin, Union Saint-Gilloise
Kundi E: Manchester United, Real Sociedad, FC Sheriff, Omonia Nicosia
Kundi F: Lazio, Feyenoord, FC Midtjylland, SK Sturm Graz
Kundi G: Olympiakos, Qarabag, Freiburg, Nantes Kundi H: Red Star Belgrade, Monaco, Ferencvaros TC, Trabzonspor
Leave a Comment