Kaka mkubwa wa Paul Pogba, Mathias Pogba ametoa video akiahidi kufichua siri kubwa ya kushtua kumhusu mdogo wake.
Mathias kupitia ukurasa wake wa Tik Tok alieleza kwamba ulimwengu unahitaji kumtambua kaka yake kwa njia tofauti.
Pogba mara nyingi amekuwa akisifiwa kama mmoja wa viungo bora licha ya baadhi ya watu wakimkosoa kuwa ameshindwa kutimiza kiwango chake kamili.
Aliwajibika pakubwa katika pambano la Ufaransa hadi kushinda Kombe la Dunia la mwaka wa 2018 nchini Urusi.
Lakini kutokana na sauti ya kaka yake huenda mashabiki wakabadilisha namna wanavyomuenzi kiungo huyo mwenye kipaji.
“Dunia nzima, pamoja na mashabiki wa kaka yangu, na hata zaidi timu ya Ufaransa na Juventus, wachezaji wenzake na wafadhili wake wanastahili kujua mambo fulani. Ili kufanya uamuzi sahihi ikiwa anastahili pongezi, heshima na upendo wa umma.” “Ikiwa anastahili nafasi yake katika timu ya Ufaransa na heshima ya kucheza Kombe la Dunia. Ikiwa anastahili kuwa mwanzilishi katika Juventus. Ikiwa ni mtu anayeaminika, mchezaji yeyote anastahili kuwa upande wake,” alisema.
Mchezaji mwenza wa Pogba katika timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe pia ametajwa na Mathias katika ufichuzi wake.
Baadaye alichukua nafasi ya wakala wa Pogba kufuatia kifo cha Mino Raiola ambaye pia alitajwa kwenye video ya Mathias.
Leave a Comment