Sports/Michezo

Kocha mpya kutangazwa Chelsea

KOCHA MPYA KUTUA CHELSEA
Written by admin

Graham Potter anatarajiwa kutangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea Ijumaa hii,baada kuifunza Brighton kwa miaka mitatu.

Potter, aliye na umri wa miaka 47 wameafikiana na mmiliki wa klabu hiyo Todd Boehly saa chache baada ya kutimuliwa kwa Thomas Tuchel.

Chelsea wanapania kumtangaza meneja mpya kabla ya mchuano wao wa Jumamosi dhidi ya Fulham.

Chelsea inakalia nafasi ya sita ligini na tayari wamefanya mazungumzo na mameneja kadhaa wakiwemo Mauricio Pochettino wa Tottenham Ruben Amorim kutoka Sporting Lisbon katika hekaheka za kumtafuta mrithi wa Tuchel.

Potter ambaye zamani alikuwa na klabu ya Ostersunds FK ya Sweeden na klabu ya Swansea ,alijiunga na Brighton alipoisaidia kumaliza katika nafasi ya tisa ligini msimu uliopita.

About the author

admin

Leave a Comment