Kocha mkuu wa AFC Leopards Patrick Aussems anatarajiwa kutua nchini Alhamisi tayari kwa msimu mpya wa mwaka 2022/2023, kulingana na katibu mkuu Gilbert Andugu.
Kocha huyo anayeishi nchini Ufaransa na familia yake alitarajiwa kujiunga na kikosi cha Ingwe mnamo Agosti 12 lakini akaomba klabu kubadili siku yake ya kusafiri.
Kulingana na Andugu, kuchelewa huko kulitokana na uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kwa kuwa kocha huyo alikuwa akipima mawimbi ya hali ya kisiasa nchini.
Mbelgiji huyo aliondoka nchini mnamo Juni 2 akielekea Ufaransa kwa likizo, kabla hata msimu kukamilika, na naibu wake Tom Juma kuchukua majukumu ya kuingoza timu hiyo kwa mechi zilizokuwa zimesalia.
Mwezi jana Aussems alitoa masharti ambayo lazima yatimizwe kabla yake kurejea katika klabu hiyo.
Kocha huyo alisema kuwa lazima AFC Leopards ilipe malimbikizi yake ya mishahara kwanza.
Leave a Comment