Sports/Michezo

Man united wapigwa na mshangao…????

United kifaa butuu
Written by admin

Kiungo wa Uholanzi Frenkie de Jong amefichua kuwa hakutaka hata kidogo kujiunga na Manchester United katika dirisha la uhamisho lililopita licha ya mustakabali wake katika klabu ya Barcelona kutojulikana.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 alionekana kuwa njiani kuondoka “Camp Nou” huku akidai Barcelona malimbikizi ya mshahara kwa kima cha yuro milioni 17.

United ilimtaka sana De Jong kocha Erik ten Hag akilenga kuduma zake lakini kiungo huyo alipambana kwa udi na uvumba kusalia Barcelona.

Yakijiri hayo Beki wa Real Madrid Antonio Rudiger ameelezea mshangao wake baada ya kuona kocha Thomas Tuchel akitimuliwa na klabu ya Chelsea.

Rudiger alitumika kama mchezaji wa akiba chini ya kocha Frank Lampard lakini Tuchel alipotua Stamford Bridge, alitokea kuwa ngome kwa the Blues. Na baada ya kuondoka mwishoni mwa msimu kwenda Real Madrid kama mchezaji huru, Rudiger ameshangazwa na waajiri wake wa zamani kumpiga kalamu Tuchel.

About the author

admin

Leave a Comment