Arsenal wameripotiwa kumtambua mshambuliaji wa Sevilla raia wa Moroko, Youssef En-Nesyri (24), kama mbadala bora wa mda mrefu wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang (32), japo mchezaji huyo ameazimia kukaa katika kilabu hiyo ya Uhispania.
Hata hivyo Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amefurahia Ainsley Maitland-Niles kusalia na Gunners akifichua kuwa alifanya mazungumzo ya faragha na kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 baada ya kiungo huyo wa Uingereza kuelezea hadharani hamu ya kuondoka klabuni hapo majira ya joto.
Arteta alidokeza kiungo wa Uingereza Jack Wilshere, 29, anaweza kufanya mazoezi na klabu yake hiyo ya zamani, Arsenal, wakati anajaribu kupata klabu mpya kufuatia kuachiliwa kwake kutoka Bournemouth.
Leave a Comment