Sports/Michezo

MICHEZO: PIGO LA AFCON KWA EPL!!!

PICHA/mtandao
Written by admin

Jumla ya wachezaji 38  kutoka ligi kuu Uingereza  watashiriki makala ya 33 ya dimba la mataifa ya Afrika AFCON nchini Cameroon, baina ya Januari 9 na Februari 6 mwaka huu.

Hata hivyo timu nne (Leeds United, Tottenham, Newcastle United na Norwich City) pekee kati ya 20 zinazoshiriki ligi kuu Uingereza  ndizo hazina wachezaji wa Afrika na hivyo basi hazitaathirika.

Arsenal, Crystal Palace, Leicester City na Watford ndizo zitaathirika pakubwa  kila moja ikipoteza wachezaji wanne.

Ivory Coast ndiyo timu yenye wachezaji wengi zaidi wa EPL wakiwa 7, ikifuatwa na Ghana na Nigeria kwa wachezaji 6 kila moja, huku  Senegal ikiwa na wanandinga  watano.

Kulingana na sheria za FIFA wachezaji wote wanapaswa kuruhusiwa kujiunga na timu za taifa kuanzia leo.

About the author

admin

Leave a Comment