Shirikisho la michezo nchini AK limetoa kalenda nyingine ya matukio yake baada ya kuahirishwa kwa muda wa wiki mbili kutokana na kifo cha mwanariadha Agnes Tirop.
Kulingana na kalenda ambayo imetolewa na naibu rais wa shirikisho hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa mashindano kwenye AK, Paul Mutwii, kaunti ya Machakos itakuwa ya kwanza kuandaa msururu huo wa mashindano ya mbio za nyikani mnamo Novemba 6.
Mashindano ya pili yatafanyika Novemba 12 mjini Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet huku kipute cha tatu kikifanyika mjini Olkalou kaunti ya Nyandarua Novemba 20.
Kapsokwony ambayo ipo katika kaunti ya Bungoma itakuwa ya nne kuandaa mashindano ya mbio hizo Novemba 27 huku kaunti ya Bomet ikiandaa mbio za mwisho wiki moja baadaye.
Leave a Comment