Mkufunzi wa klabu cha Arsenal Mikel Arteta amepania kumkuza kiungo wa kati wa timu ya wachezaji chipukizi katika klabu hiyo Charlie Patino (17) katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo licha ya tetesi kudokeza Barcelona inamnyatia mchezaji huyo wa Uingereza kwa mujibu wa Mirror.
Barcelona imetia nia kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba (28) katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao kwa kuzingatia kama tu hatotia saini kandarasi mpya na Man United.
Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya wanatarajia ushindani mkubwa kutoka klabu za PSG, Juventus na Real Madrid kwa mujibu wa Fichajes ya Uhispania.
Huku hayo yakisubiriwa, kwa mujibu wa SportBild ya Ujerumani, Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner (25) ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaofukuziwa na Borussia Dortmund kufuatia tetesi za mshambuliaji matata wa klabu hiyo Erling Braut Halaand kutaka kuondoka Signal Iduna Park msimu ujao.
Leave a Comment